Licha ya Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto wa mwaka 1989 kuweka wazi kwamba ni kosa la kisheria kumfanyia mtoto ukatili, bado vitendo hivyo vinaonekana kushamiri, hasa katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, ukiwemo Mwanza ambapo Global TV imefanikiwa kukutana ana kwa ana na watoto 29 waliofanyiwa vitendo vya kikatili, ikiwemo kupigwa vikali, kujeruhiwa au kumwagiwa maji ya moto. Mwandishi wetu, Catherine Kahabi amefunga safari mpaka kwenye Kituo cha Foundation Karibu Tanzania, wanakohifadhiwa watoto waliofanyiwa ukatili, na ifuatayo ni ripoti yake: