×

Shigongo Atoa Somo kwa Wanavyuo na Vijana kwenye Victory Campus Night 2017 (Video + Picha)

Shigongo akizungumza kwenye tamasha hilo.
Akifafanua jambo
Umati wa watu ukimshangilia Shigongo
Mchungaji Samuel akitoa neno

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shogongo amehudhuria Tamasha la Campus Night lililowakutanisha wanafunzi wa vyuo na vijana uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika Viwanja vya Tanganyika Packers uliopo Kawe jijini Dar.

Akiongea na wanafunzi hao, alisema kuwa amefurahi kuwaona wanafunzi hao wakifika kwa wingi katika tamasha hilo na kuwataka wasishangae kuona watoto wadogo wakifanya mambo makubwa katika jamii huku akisema kuwa ni zama za vijana kufanya makubwa.

Alisisitiza kuwa vijana ndiyo watu wanaotakiwa kufanikiwa kipindi hiki huku akiwaambia akili za binadamu wa leo zimebadilika sana tofauti na watu waliopita huko nyuma. Kwa binadamu wa sasa uwezo wake wa kufikiria ni mpya na uwezo wa kuchunguza mambo ni mpya kwa sababu ya mazingira ya leo, ndo sababu ukikutana na vijana wa sasa wanaweza ku-challange vitu kulinganisha na watu wa karne ya 20.

Pia aliwataka wanavyuo na vijana kujisomea vitabu ili kujifunza maarifa mapya kila kukicha.

Leave a Comment