Msanii wa Bongo Fleva, Haitham Kim anayetamba na kibao chake cha ‘PlayBoy’ alichomshirikisha Queen wa Bongo Muvi, Wema Sepetu, amemlipua aliyekuwa meneja wake ambaye ni Producer wa Studio ya MJ RECORDS, Daxo Chali, baada ya kutangaza kuwa ameacha kuwasimamia kwenye mtandao wa kijamii bila kuwapa taarifa yeye na msanii mwenziye anayeitwa Nini.