The House of Favourite Newspapers

Uzinduzi Wa Filamu Ya Mobeto, Zero Player Wafunika (Pichaz + Video)

0
Mwanamitindo, Hamisa Hassan Mobeto akiwa kwenye Red carpet ya uzinduzi ya Filamu  yake iitwayo Zero Player, shughuli iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa Quality Centre jijini Dar.
…Akiwa katika pozi.
Mwanamitindo, Hamisa Mobeto akiwa katika picha ya pamoja na Mama wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa (katikati) na mdogo wa mareheku Kanumba, Seth Kamugisha Bosco.
…Akiwa na Shabiki wake.
…Picha zikiendelea
Mobeto akiongea na mashabiki wake.

MWANAMITINDO  Hamisa Hassan  Mobeto, usiku wa kuamkia leo amezindua rasmi filamu yake iitwayo Zero Playe, shughuli iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa Quality Centre jijini Dar na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali pamoja na wadau wa burudani.

 

Filamu hiyo ambayo imeandaliwa nchini, Afrika Kusini, Mobeto ameigiza kama Mhusika mkuu huku akitumia jina la Jack, akiwa sanjari na Seth Bosco, mdogo wa marehemu Steven Kanumba, Seth Bosco.

Akizungumzia uzinduzi huo, Mobeto alisema filamu hiyo ilianza kuandaliwa mwaka jana na sababu za kucheleweshwa kuzinduliwa ni kwa sababu ya ujauzito wake, hivyo ilikuwa ni lazima waandaaji wasubiri muda wake wa kujifungua hadi hapo jana ulipofanyika uzinduzi huo.

 

Mbali na uzinduzi wa filamu hiyo, Mobeto alisema katika maisha yake huwa haumizwi na maneno ya watu labda pale mzungumzaji anapowahusisha watoto wake na mama yake.

 

“Filamu hii ilianza kuandaliwa mwaka jana, lakini ilipokamilika tayari nilikuwa na ujauzito hivyo ikawalazimu kusubiri hadi nijifungue salama hadi leo ilipotimia, lakini niseme ukweli kwamba huwa siumizwi na maneno ya watu labda pale yanapowahusisha wanangu na mama yangu, hapo kidogo huwa natikiswa,” alisema Mobeto.

(PICHA: GLOBAL TV ONLINE)

Leave A Reply