×

UJUMBE MZITO WA BARNABA KWA MZAZI MWENZIYE!

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barnaba Boy

HIT maker wa ngoma ya ‘Mapenzi Jeneza’, Barnaba Boy, amemuandikia ujumbe mzito mzazi mwenziye, Zuu Namela, katika siku yake ya kuzaliwa, ambao mashabiki wameufasiri kama Mbongo Fleva, huyo moyo wake umebeba maumivu na anatamani kurudiana na mzazi mwenziye.

 

Barnaba na Zuu Enzi ya Penzi Lao

Barnaba aliandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram, akimtakia mzazi mwenziye huyo maisha marefu na aendelee kutabasamu milele hata kama tabasamu hilo halitengenezi yeye, kutokana na Zuu tayari ameshaanzisha uhusiano na Mbongo Fleva mwingine anayeitwa Brown.

Baada ya Posti yake hiyo mashabiki hawakusita kutiririka na kukomenti huku wengi wao wakisema kuwa Barnaba anaumia sana, sema tu hana la kufanya ili kumrudisha mzazi mwenziye huyo ambaye amekufa, ameoza kwa mpenzi wake mpya wa sasa.

Zuu Namela Akiwa na Mpenzi Wake wa Sasa, Brown

Barnaba na Zuu waliwahi kuwa wapenzi na kuishi pamoja, wakabarikiwa kupata mtoto mmoja anayeitwa Steve, lakini baadaye penzi hilo liliingia shubiri wakatengana.

Na Isri Mohamed/GPL

Leave a Comment