
STAA mkali wa filamu Aunt Ezekiel, ameweka wazi nia yake ya kufunga ndoa yake ya pili na mzazi mwenzie Moses Iyobo, na kusisisitiza kuwa wakati umefika.
Akizingumza na Kilinge, Aunt alisema kuwa muda waliokaa na mzazi mwenzie huyo unatosha kabisa kufunga naye pingu za maisha, kwa sababu wameshajuana vilivyo.
“Unajua huko nyuma nilikuwa sina wazo kabisa na ndoa lakini sasa n i k o tayari na wakati wowote kuanzia sasa watu watasikia,” alisema Aunt ambaye wamebahatika kuzaa mtoto wa kike n a mcheza dansa huyo.
Ndoa ya kwanza ya Aunt alifunga na Sunday Demonte kabla ya kuachana.
Stori: Imelda Mtema | Championi Jumatatu