×

Binti Mfalme Martha Louise wa Norway Kuolewa na Mganga

Shamrashamra za harusi ya Binti Mfalme Martha Louise wa Norway zimeanza rasmi baada ya miaka mingi ya misukosuko.

Martha (52) na mpenzi wake ambaye ni Mfanyabiashara na Mganga wa asili (Mganga wa jadi) huko Marekani Durek Verrett (49) wanatarajia kufunga ndoa Jumamosi ya wiki hii katika mji wa Geirager.

Mamia ya wageni wakiwemo watu mashuhuri wameanza kuwasili nchini Norway kwa ajili ya shughuli za harusi hiyo kubwa.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Norway, wageni waalikwa wameombwa kutotumia simu zao wala kamera wakati wa sherehe hizo na kutoposti chochote kwenye mitandao ya kijamii.

Maisha ya Binti huyo yamekuwa yakizungukwa na utata mwingi kwani kuna nyakati ambazo amefanya mambo yaliyolazimu kuvuliwa cheo cha Kifalme.

Mwaka 2002 alianzisha Biashara yake mwenyewe kinyume na sheria za kifalme, mwaka 2007 alitangaza kuwa na uwezo usio wa kawaida wa kuona hisia au matukio ya siku zijazo.

Aidha mwaka 2018 alianzisha shule ambapo alisema atawafundisha watu kutengeneza miujiza na kuongea na Malaika.

Wakati huohuo, Mume wake mtarajiwa ni mganga wa asili ambaye hujiita mtumishi wa Mungu mwenye nguvu zisizo za kawaida.

Mganga huyo ambaye hajakubalika sana nchini Norway , anadai kuwa alifufuka kutoka kwa wafu na akiwa mdogo ndugu yake aliwahi kumtabiria kuwa siku moja atamuoa binti mfalme wa Norway.

MSTAAFU KIKWETE – RC CHALAMILA WAKIFUATILIA RAIS SAMIA AKITUNUKU NISHANI ya MIAKA 60 ya JWTZ

Leave a Comment