×

Emmerson Mnangagwa Aapishwa Rais Mpya Zimbabwe

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu.
…Akipigiwa wimbo wa taifa baada ya kuapishwa.
Askari wakipiga mizinga ya heshima katika uapisho huo.
Rais Mnangagwa na mkewe Auxillia wakiwa wakiwasalimia wananchi waliofika uwanja ambao aliapishwa.
Wananchi wakiwa na mabango ya kumpongeza Rais Mnangagwa.

HATIMAYE Zimbabwe imempata rais mpya, Emmerson Mnangagwa, ambaye ameapishwa rasmi kuchukua wadhifa huo kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe aliyeliongoza taifa hilo kwa miaka 37 tangu  lijipatie uhuru kutoka wa Waingereza.

Kifuatacho ni kiapo cha Emmerson Mnangagwa alichokitoa leo:

”Mimi Emmmerson Dambudzo Mnangagwa naapa kwamba kama Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe nitakuwa muaminifu kwa Zimbabwe na kuheshimu na kuilinda katiba pamoja na sheria zingine zote za Zimbabwe na nitalinda sheria zote zitakazoendeleza nchi hii na nitapinga chochote kitakachoiathiri Zimbabwe na nitalinda na kuimarisha haki za watu wa Zimbabwe na  nitatekeleza majukumu yangu kwa nguvu zangu zote na uwezo wangu wote na nitaheshimu haki za Zimbabvwe na raia wake, ewe mwenyezi Mungu nisaidie”.

Upinzani unamtaka  Mnangagwa, ambaye amekuwa mmoja wa watawala, kumaliza “utamaduni wa ufisadi”. Taarifa ya kuondoka madarakani kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93  Jumanne iliyopita iliibua sherehe kubwa kote nchini Zimbabwe.

Leave a Comment