Rais Magufuli Atembelea Meli Ya Hospitali Ya China
Global Publishers November 26, 2017 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, akikagua gwaride la wanamaji wa Meli ya Hospitali ya China (Ark of Peace) alipoitembelea leo kuwashukuru na kuwaaga baada ya kutoa huduma kwa wananchi kwa takriban juma zima katika bandari ya Dar es Salaam. …Akikagua gwaride la wanamaji na wanaanga wa meli hiyo.
Akitembezwa sehemu mbalimbali na kiongozi wa meli hiyo, Kamanda Guan Bailin.
Rais John Magufuli leo ameitembelea na kuwaaga wanajeshi wa Meli ya Hospitali ya Jeshi la Maji la China ambayo imekuwa nchini kwa takriban juma zima ikitoa matibabu na uchunguzi kwa Watanzania kwa magonjwa mbalimbali. Meli hiyo ilikuwa imetia nanga katika bandari ya Dar es Salaam.