
UONGOZi wa Yanga umesema kuwa kambi yao ya nje ya nchi ipo palepale na kikubwa wanachosubiria ni droo ya Ligi ya Mabingwa afrika inayotolewa na Shirikisho la Soka afrika (Caf).
Awali, Yanga ilipanga kwenda kuweka kambi yake nchini China kwa ajili ya matayarisho ya msimu mpya baada ya kukamirisha zoezi lao la usajili.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano, Franky Kamugisha alisema ratiba ya Caf itakayotolewa baadaye mwezi huu ndiyo itaamua nchi gani watakayokwenda
kuweka kambi.

“Hatufanyi vitu kwa kujionyesha au kutaka sifa, sisi tunafanya vitu kwa mipango, awali tulitangaza kwenda kuweka kambi nje ya nchi lakini baadaye tukabadili tukisubiria ratiba ya Caf ili kujua tutaanza kucheza na
timu gani.
“Na lengo kubwa ni kwenda kuweka kambi kwenye nchi itakayoendana na hali ya hewa na mazingira halisi kutoka kwenye timu tuliyopangiwa na Caf baada ya droo kuchezeshwa,” alisema Kamugisha.