
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imekutana na watangazi wa radio mbalimbali nchini na kuongelea ongezeko la faida za mteja katika huduma za intaneti zinazotolewa na Airtel kupitia kuzinduliwa kwa bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zilizozinduliwa mwanzoni mwa wiki hii kwa lengo lengo la kuwapatia wateja na watumiaji wote wa intaneti bando nafuu zaidi.
Meneja Masoko Airtel Tanzania Anethy Muga alieleza kuwa bando Mpya ya ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zinatoa uhuru kwa wateja wote kujichagulia bando la intaneti KABAMBE wakati wowote, na kusisitiza kuwa mteja wa Airtel ataweza kunufaika na SMATIKA na Yatosha Intaneti kwa kujipatia bado za gharama nafuu ya hadi shilingi 200 na kupata MB 40. Vilevile ofa kabambe ya ‘SMATIKA Yatosha bando’ itamuwezesha mteja wa AirtelKUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu”

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Yatosha mpya inakupa bado za siku, wik, mwezi gharama nafuu kuliko zote nchini, kwa mfano bado ya 5,000 zamani ilikuwa na GB 1, kwa sasa Yatosha Intaneti Mpya unapata GB 2 kwa siku 7, vile vile kwa shilingi 10,000 zamani ulikuwa unapata bando la GB 2.5 kwa siku 7 lakini sasa tumeliongeza zaidi unapata GB 6 zakutumia wiki nzima. Alieleza Muga
“SMATIKA na Yatosha Intaneti’ ni ishara ya Airtel kuanza vyema shamrashamra kusherehekea sikukuu kwa kuwapatia uhakika wateja na watumiaji wa huduma ya intaneti wa kutoishiwa bando kwa muda mfupi, Ukiwa na Airtel Yatosha Intaneti hainaga kuzima data tena!” Alisisitiza Mmbando.
HADITHI: SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU – SEHEMU YA 1 (Audio)
Nakuletea dakika 15 za kwanza za simulizi hii tamu ya SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU. Ukitaka kuisikiliza simulizi hii Install #GlobalPublishersApp sasa. Utasoma na kusikiliza kitabu chote kuanzia sehemu ya kwanza hadi ya mwisho bureeeee!
Android: Bofya ==>http://bit.ly/2AAQe1d
iOS: Bofya ==>http://apple.co/2Assf4M