×

FT: MBAO FC 2-0 YANGA UWANJA WA CCM KIRUMBA, MWANZA

Kikosi cha timu ya Mbao FC.

FULL TIME

Dk ya 94: Mwamuzi anamaliza mchezo, Mbao wanaendeleza rekodi ya kuifunga Yanga mfululizo, wanaibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Dk ya 90: Zinaongezwa dakika 4.

Dk ya 89: Mambo bado ni magumu kwa Yanga.

Dk ya 84: Yanga wanafanya shambulizi kali, Pius Buswita anashindwa kumalizia kazi nzuri waliyoifanya.
Dk ya 84: Yanga wanafanya shambulizi kali, Pius Buswita anashindwa kumalizia kazi nzuri waliyoifanya.
Dk ya 83: Upinzani umekuwa mkali.

Dk ya 80: Yanga wanapambana kutafuta bao la kusawazisha.

Dk ya 76: Beki wa Mbao, David Mwasa anapata kadi ya pili ya njano. Anatoka nje, sasa Mbao wako pungufu.

Dk ya 72: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Papi Tshishimbi anaingia Yusuph Mhilu.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dk ya 65: Mbao wanamtoa James Msuva, anaingia Boniface Maganga.

Dk ya 60: Mbao wanafanya mashambulizi makali mara mbili mfululizo.

Dk ya 57: Mwashiuya anaingia, anatoka Emmanuel Martine.

Kikosi cha timu ya Yanga.

Dk ya 53: Mbao FC wanapata bao la kwanza kupitia kwa Habib Haji ambaye anapiga shuti kali la nje ya eneo la 18.

Dk ya 57: Mwashiuya anaingia, anatoka Emmanuel Martine.

Dk ya 53: Mbao FC wanapata bao la kwanza kupitia kwa Habib Haji ambaye anapiga shuti kali la nje ya eneo la 18.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dk ya 47: Mbao wanatulia na kujipanga.

Dk ya 45: Yanga wameanza kwa kasi, Martine anafanya shambulizi lakini mpira unatoka.

Kipindi cha pili kimeanza.

MAPUMZIKO

Dk ya 45 + 49: Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza.

Dk ya 45: Zinaongezwa dakika nne za nyongeza.

Dk ya 42: Mbao wanafika langoni mwa Yanga lakini umakini wa walinzi unasaidia.
Dk ya 41: Tshishimbi anapiga shuti linapaa juu ya lango.

Dakika ya 36: Yanga wanafanya shambulizi kali lakini walinzi wa Mbao wanaokoa inakuwa kona ambayo haina faida.

Dakika ya 34: Mchezaji wa Mbao FC, George Sangida anapata kadi ya njano kwa kucheza faulo dhidi ya Pius Buswita wa Yanga.

Dakika ya 32: Mbao wanafika langoni mwa Yanga lakini mpira wa krosi unadakwa vizuri na kipa Youthe Rostand.

Dakika ya 30: Mashabiki wanashangilia kwa nguvu, mpira unachezwa katikati ya uwanja muda mwingi.

Dakika ya 27: Mbao wanaendelea kumiliki mpira lakini Yanga wanafanya mashambulizi ya kushtukiza.

Dakika ya 23: Mbao wanacheza soka la pasi, wanaelewana, wapanatapa shangwe za nguvu kutoka kwa mashabiki wao.

Dakika ya 21: Yanga wanatengeneza nafasi kadhaa lakini bado mambo magumu.

Dakika ya 15:Inapigwa inakuwa kona nyingine lakini inaokolewa.

Dakika ya 14: Mbao wanafika langoni mwa Yanga, mpira unatoka inakuwa kona.

Dakika ya 10: Mbao wanaanza kucheza kwa kujiamini.

Dakika ya 6: Mbao FC wanapata kona, inapigwa inaokolewa.

Dakika ya 1: Mchezo umeanza kwa kasi kiasi.

Mchezo unaanza.

Mchezo unatarajiwa kuanza muda wowote kutoka sasa. Timu zimeshaingia uwanjani, ni ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Huu ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga wapo ugenini kukutana na Mbao FC.

Kikosi cha Young Africans kitakachoanza dhidi ya Mbao FC, leo;

1. Youthe Rostand

2. Juma Abdul

3. Gadiel Michael

4. Abdalah Shaibu

5. Vicent Andrew

6. Pato Ngonyani

7. Pius Buswita

8. Papy Tshishimbi

9. Amis Tambwe

10. Raphael Daudi

11. Emmanuel Martin

Kikosi cha akiba

12. Ramadhan Kabwili

13. Hassan Kessy

14. Haji Mwinyi

15. Nadir Haroub

16. Said Juma

17. Yusuph Mhilu

18.Geofrey Mwashiuya