×

YANGA Watengewa MIL 200 Kuwafunga SIMBA – Video

UONGOZI wa Yanga na mdhamini GSM wamehaidi kutoa Sh 200milioni kwa wachezaji wa Yanga iwapo watashinda mechi yao dhidi ya Simba Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa.

Akizungumza makao makuu ya Yanga, Afisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz alisema wadhamini wa GSM wameweka mezani Sh200 Milioni kwa wachezaji endapo watapata ushindi wa aina yoyote siku hiyo.

 

“Hata wakichukua ubingwa sio tatizo, tunachohitaji ni kuwachapa, nadhani raha ya ubingwa utakuwa umeisha na kuwanyamazisha kupiga kelele hovyo mtaani.

 

“Tulikuwa na utaratibu wa kutoa motisha kila wanaposhinda kwenye michezo ya Ligi Kuu hupewa Sh 10Milioni, lakini kutokana na umuhimu wa mchezo wa Jumapili tumeamua kufanya kitu kwa wachezaji ili kuweka raha Jangwani,’ alisema Nugaz.

 

Aliongeza kocha, Luc Eymael amemweleza kuwasoma Simba kwa muda mrefu tangu alipowasili nchini kukinoa kikosi hicho na amegundua mambo mengi ya kuwadhibiti wapinzani wao.

Leave a Comment