
MICHUANO ya Soccer Beach inayodhaminiwa na gazeti namba moja la michezo Tanzania la Championi na Kampuni ya Kubashiri Michezo ya Kubahatisha ya Sokabet Tanzania inatarajiwa kuendelea kesho na Jumamosi.
Soccer Berach ambayo inashirikisha timu 16 za vyuo mbalimbali hapa nchini leo itaendelea kwenye fukwe za Coco, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ratiba za mechi za kesho Jumamosi IFM itafungua mashindano hayo kwea kuvaana na HKMU saa nne kamili asubuh.

Mechi nyingine zitakazofuata ni TIA itakayomenyana na DSJ saa tano kamili asubuhi kabla ya kuingia DIT watakaovaana na AMCET saa nane mchana.
Na saa tisa kamili Ardhi wataingia uwanjani kukipiga na CBE mchezo unaotarajiwa kujaa upinzani mkubwa kutokana na upinzani unaokuwepo wakati wanapokutana.
Mashindano hayo yanaendelea Coco baada ya mapumziko ya wiki mbili na nusu ili kupisha mithiani ya wanafunzi hao waliyokuwa wanafanya.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeweka mkazo katika soka la ufukweni sambamba na lile la wanawake ili kuleta maendeleo katika upande huo wa soka na vijana.