The House of Favourite Newspapers

Madaktari wa Kairuki Wagongwa 10-3

Timu ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki dhidi ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), zote za jijini Da es Salaam zikitifuana vilivyo.
Mechi hizo zikitifuana vilivyo.

 

Kipa akijiandaa kuudaka mpira.
Mchezaji akiwa chini huku akionyesha ujanja wake.

 

TIMU ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, imejikuta katika wakati mgumu baada ya kupokea kichapo kikali cha mabao 10-3 dhidi ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), zote za jijini Da es Salaam katika mchezo wa Michuano ya Ligi ya Soka la Ufukweni ‘Beach Soka’ inayoendelea jijini.

 

Katika mchezo huo ambao ulipigwa mapema leo kwenye Ufukwe wa Coco, IFM walionyesha uwezo mkubwa katika kumiliki mpira huku wakipiga mashuti makali yaliyopelekea kupata ushindi huo mnono na kuwafanya watinge katika hatua ya nusu fainali itakayochezwa kesho Jumapili hapohapo Coco.

 

Gazeti la Championi na Kampuni ya Kubashiri matokeo ya Sokabet ni kati ya wadhamini wa michuano hiyo.

 

NA MUSA MATEJA/GPL

Comments are closed.