


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla umempa masaa mwanamme mmoja anayedaiwa kumdhurumu mpenzi wake kiwanja na nyumba kutokana na kwamba mwanaume huyo alitafuta wakili na kufoji nyaraka za kuonyesha mwanaume huyo ni sehemu ya umiliki na uendelezaji wa eneo hilo ambapo wakili huyo pasipokuwa makini alitumia sheria ya jiji la California nchini Marekani katika mikataba hiyo feki inayoonesha kutaka kumtapeli.
Mhe. Makalla amewataka Madiwani na Maafisa watendaji Kata kutatua kero za wananchi kwa vitendo inayowasumbua wananchi ambapo ametaka kila mtumishi kuhakikisha anashughulikia kero za wananchi.
Kuhusina na mgogoro huo Mkuu wa Mkoa amekabidhi Jambo hilo kwa Vyombo vya vya dola kwaajili ya kulishughulikia kwa mujibu wa Sheria leoleo ili mwanamke huyo ambaye alinunua kiwanja hicho kihalali aweze kupata haki yake.
Aidha RC Makalla ametatua Mgogoro wa Mwananchi aliejenga Ukuta na kuziba Barabara za kuingia kwenye makazi ya watu ambapo amemuelekeza Afisa Ardhi Kinondoni kumaliza Mgogoro huo kwa kumuelekeza aliyeziba Barabara kuvunja na kuachia Barabara.
Pamoja na hayo RC Makalla amewapatia Madiwani na Maafisa watendaji Kata ajenda za kushughulikia ambapo miongoni mwa hizo ni kuimarisha Ulinzi na Usalama wa Wananchi, Usafi endelevu wa Mazingira, Makusanyo ya Mapato na usikilizaji wa kero za Wananchi.
Agenda nyingine alizotoa RC Makalla ni usimamizi wa miradi ya maendeleo, Manispaa kutenga asilimia 10 ya mikopo kwa Vijana, Walemavu na Wanawake pamoja na kujenga umoja na mshikamano wa kazi miongoni mwa Watendaji na kuepuka Migongano na Mivutano.