The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Kibatala Ajiengua Kesi ya Wema, Msando Akomaa Nayo

WAKILI Peter Kibatala ameiandikia barua Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akiomba kujitoa kumuwakilisha Diva wa Bongo Movies, Wema Sepetu katika kesi ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi inayomkabili mahakamni hapo.

 

Maamuzi hayo ya Kibatala yameelezwa leo Jumatano, mahakamani hapo, baada ya wakili huyo kushindwa kuendelea kusikiliza kesi hiyo. Aidha mahakama hiyo imepokea barua kutoka kwa Wakili Albert Msando kuomba kumuwakilisha Wema katika kesi hiyo na kwamba aliomba apewe muda wa kupitia jalada hilo kabla ya kuendelea na kesi.

 

Hata hivyo, hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba anayesikiliza shauri hilo, amesema kuwa amepokea barua hizo Januari 9, mwaka huu na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 8, 2018, itakaposikilizwa tena. Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Angelina Msigwa  na Matrida  Abbas.

VIDEO: Kilichotokea Mahakamani Kwenye Hukumu ya Scorpion Leo

Comments are closed.