Mgogoro nwa kimaslahi kati ya halmashauri ya mji wa Njombe na mkandarasi Masasi Construction, unaeleza kukwamisha ujenzi wa kituo cha mabasi cha mkoa wa Njombe, uliogharimu shilingi Bilioni 2 na Milioni 800.
Mkuu wa mkoa wa Njombe, Christopher Olesendeka, ametoa siku 3 kwa pande zinazohusika kumaliza mgogoro huo na ujenzi wa kituo hicho cha mabasi uweze kuendelea ili kuhudumia wananchi.