



Serikali za Tanzania na China, zimefikia makubaliano ya kuanzisha kikosi kazi cha pamoja kwa ajili ya kuyafanyia kazi makubaliano yaliyofikiwa na nchi hizo mbili katika kuboresha sekta ya kilimo nchini.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo na waziri mwenzake wa kilimo kutoka nchini China Dkt, Dongqu Quphd ambapo amesema wamejadiliana kuhusu wakulima wa Tanzania wanavyoweza kunufaika na soko la mazao nchini China pamoja na namna ya kuboresha kilimo nchini Tanzania.
Waziri Tizeba amesema wamekubaliana na naibu wake, Mary Mwanjelwa, asafiri kwenda nchini China katikati ya mwezi Mei, mwaka huu kuhudhuria maonyesho ya bidhaa za kilimo na kwenda kutilia mkazo mambo waliyokubaliana ikiwemo suala la uwekezaji.
Dkt. Tizeba amesema katika mazungumzo hayo wamekubaliana kuwa na ushirikiano wa kitaaluma kati ya wanasayansi wa china na wa kitanzania katika taaluma yakilimo kwa kubadilishana uzoefu wa taaluma ya kilimo.
NA DENIS MTIMA/GPL