The House of Favourite Newspapers

Makonda Aanza Kusikiliza Kero za Waliodhulumiwa Nyumba – Video

MKUU wa Mkoa wa Dares Salaam, Paul Makonda, leo ameanza kusikiliza kero mbalimbali zinazohusu masuala ya migogoro ya ardhi  na watu waliodhulumiwa nyumba zao kwa kuwapatia msaada wa kisheria.

Baadhi ya wananchi waliofika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa nje wakisubiri kuhudumiwa matatizo yao.

Akizungumza na wakazi wa mkoa wa wake, Makonda amesema  anatambua wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam wamekuwa wakiteseka kutokanana kudhulumiwa ardhi na nyumba katika maeneo mbalimbali.

 

Pia ameongeza kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu kwa wiki nzima ili kusikiliza na kutatua matatizo yanayowasumbua wakazi wa mkoa wake.

 

Nao baadhi ya wakazi wa mkoa huo waliofika katika ofisi zake waliozungumza na mtandao huu wamempongeza mkuu wa huyo wa mkoa kwa hatua anazozichukua katika kushughulikia matatizo mbalimbali ya wakazi wake.

Comments are closed.