The House of Favourite Newspapers

OKWI: MTABANA ILA MTAACHIA TU

Straika wa Simba, Emmanuel Okwi akiongea jambo na mashabiki.

 

AKIONGOZA kwa mabao 13 katika Ligi Kuu Bara, straika wa Simba, Emmanuel Okwi, amesema wana kibarua kigumu cha kuchukua ubingwa wa ligi kuu, lakini watapambana kuhakikisha wanautwaa.

 

Okwi, raia wa Uganda, ameitoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache baada ya kuifungia Simba bao pekee la ushindi dhidi ya Azam FC katika mechi ya ligi hiyo Jumatano wiki hii.

 

Katika mechi hiyo iliyojaa upinzani mkubwa, Okwi alionekana akibanwa vilivyo wakati mwingine kuchezewa kindava lakini alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi ya Asante Kwasi.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Okwi alisema licha ya kuongeza pointi katika msimamo wa ligi, lakini bado wana kibarua kigumu cha kupambana kufanikisha hilo.

 

“Hakuna kitu kizuri kinachopatikana kwa urahisi, ni lazima ugumu uwepo katika kupata mafanikio, hivyo ni lazima mimi pamoja na wachezaji tupambane ndani ya uwanja ili tufanikishe malengo yetu.

 

“Ninaamini kwa Mungu hakuna kitu kigumu, kikubwa ni kupambana kwa nguvu dhidi ya wapinzani wetu ili tufanikishe malengo yetu tuliyojipangia ikiwemo ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu.

 

“Niwashukuru mashabiki wa Simba kwa sapoti kubwa wanayotupa, kiukweli tunawaheshimu sana kwani sisi bila ya wao tusingekuwa tunapata matokeo haya na ninaamini wakiendelea hivyo basi tutafanikisha malengo yetu, tuna timu nzuri ya ubingwa,” alisema Okwi.

 

Mshambuliaji huyo, hadi hivi sasa tayari amefanikiwa kuifungia timu yake mabao 13 akiongoza katika orodha ya wafungaji akifuatiwa na Mzambia wa Yanga, Obrey Chirwa aliyepachika 10.

MAGAZETI LEO FEB 10: SIRI TATU ZA DIAMOND KUUFYATA KWA MOBETO HIZI HAPA

Comments are closed.