The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Waziri Mkuu Ethiopia Ajiuzulu

WAZIRI Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, amejiuzulu wadhifa huo baada kuandika barua kwa chama chake cha Ethiopia People’s Democratic Front akiomba kung’atuka, licha ya chama hicho kutobainisha iwapo kimekubali uamuzi wake au la.

 

Desalegn amesema kuwa amejiuzulu ili kusaidia kusuluhisha mzozo wa kisiasa uliopo nchini humo. Wananchi, wakereketwa wa Ethiopia People’s Revolutionary Democratic Front na serikali inataka kupata ufanisi wa mabadiliko yaliyowekwa wakati  wa mgogoro wa kisiasa nchini humo. Wengi wamepoteza maisha, wengine makazi huku mali zao zikiharibiwa.

 

“Ili kupata suluhu na ufanisi wa mabadiliko yaliyowekwa, na suluhu tuliyoweka,  nimewasilisha barua ya kujizulu majukumu yangu katika serikali na katika chama kwa hiari yangu,” alisema katika runinga ya taifa ya EBCTV.

JPM AKIMUAPISHA MNADHIMU MKUU WA JWTZ

Comments are closed.