×

YANGA IMESONGA MBELE KWA JUMLA YA MABAO 2-1

DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 90 Yanga inapata kona dakika za mwisho kabisa
Dk 89 shambulizi kali wanafanya St Louis, lakini Rostand anaonyesha yuko vizuri anadaka na kulala
Dk 89 Yanga wanaendelea kuonekana hawana haraka kwa kuwa uhakika sasa ni asilimia 99

Dk 84 Rostand taratibu anaonyesha mbwembwe huku akidaka na kulala chini
Dk 83 Yanga inapata kona, inachongwa kibishooo na Ajibu na kipa anadaka kwa ulaini

Dk 75 Ajibu anawachambua mabeki watatu, lakini anakuwa na haraka katika umaliziaji, goal kick
Dk 74 Rostand anaruka juu kudaka, anautema. Hatariii lakini St Louis wanakosa, goal kick

SUB Dk 59 Makapu aliumia, ameshindwa kuendelea na nafasi yake inachukuliwa na Raphael Daud Loti
SUB Dk 57 St Louis wanafanya mabadiliko wanamuingiza Mellanie

KADI Dk 55, Makapu analambwa kadi ya njano baada ya kumgonga mshambuliaji wa St Louis
Dk 54, nusura Tshishimbi aipatie Yanga bao la pili lakini anadhibitiwa

KADI Dk 55, Makapu analambwa kadi ya njano baada ya kumgonga mshambuliaji wa St Louis
Dk 54, nusura Tshishimbi aipatie Yanga bao la pili lakini anadhibitiwa
Dk 54, Kessy tena mara nyingine kutokea katikati, anaachia mkwaju mkali, lakini hakulenga lango Dk 52 Makapu anafanya kazi ya ziada na kuukoa mpira, kona kwenye lango la Yanga, inachongwa goal
Dk 49, Kessy anaingia vizuri, safari hii anajaribu mwenyewe, goal kick
Dk 47, mpira mreefu kwenye lango la Yanga, Rostand anaruka na kudaka vizuri kabisa
45 St Louis wanaanza kwa kasi kubwa wakionekana wamepania kupata bao

Kipindi cha pili kimeanza

HALF TIME
DAKIKA 1 YA NYONGEZA
GOOOOOOOO Dk 45 sekunde kadhaa baada ya Ajibu kurejea uwanjani anaunganisha krosi safi kabisa ya Kessy na kuitanguliza Yanga ya Tanzania kwa bao moja
Dk 44 Ajibu amerejea uwanjani kuendelea na mchezo

Dk 38 Kessy anaingia vizuri hapa, anavutwa lakini mwamuzi msaidizi inaonekana hakuona, Kessy anahoji

Dk 36 Yanga wanapata nafasi nzuri kabisa lakini Buswita anaonekana kama mtu aliyechoka au mgonjwa hivi!!

Dk 30 Kessy anapiga pasi safi kwa gadiel, naye anapiga mkwaju unaokolewa na kuwa kona nyingine kwa Yanga, inachongwa kona fupi, inaokolewa
KADI Dk 29 Cannavaro analambwa kadi ya njano kwa kucheza kindava
Dk 28, krosi nzuri ya Gadiel, St Louis wanaokoa lakini mpira anauwahi Ajibu anaachia mkwaju hapa, goal kick

Dk 27, mpira wa faulo, ni hatari lakini Rostand anaruka juu kabisa na kuudaka
Dk 26 Kessy anamuangusha kiungo wa St Louis, si mbalis ana karibu na lango lao
Dk 24 Martin anaachia mkwaju mkali unawababatiza w

Dk 26 Kessy anamuangusha kiungo wa St Louis, si mbalis ana karibu na lango lao
Dk 24 Martin anaachia mkwaju mkali unawababatiza walinzi wa St Louis unatoka na kuwa wa kurushwa
Dk 19, St Louis wanapata kona ya kwanza baada ya kufanya shambulizi kali. Inachongwa hapa lakini Tshishimbi anaokoa hapa
Dk 17, Yanga inapata kona nyingine baada ya krosi safi ya Ajibu. Ajibu huyohuyo anachonga kona safi kabisa lakini offside

Dk 19, St Louis wanapata kona ya kwanza baada ya kufanya shambulizi kali. Inachongwa hapa lakini Tshishimbi anaokoa hapa
Dk 17, Yanga inapata kona nyingine baada ya krosi safi ya Ajibu. Ajibu huyohuyo anachonga kona safi kabisa lakini offside
Dk 13, kona inachongwa lakini haina manufaa hata kidogo
Dk 13, Yanga wanafanya shambulizi kali na kupata kona ya pili

Dakika ya 15: Yanga wanatawala mchezo. Mashabiki siyo wengi uwanjani.

Dakika ya 9: Yanga wanafanya shambulizi, Tshishimbi anapiga krosi inaokolewa.

Dakika ya 6: Ibrahim Ajibu anapiga kona inaokolewa.

Dakika ya 5: Yanga wanafanya shambulizi kali, inakuwa kona.

Dakika ya 1: Kasi ni ndogo.

Mchezo umeanza.

Mchezo wa Klabu Bingwa Afrika, mechi ya kwanza Yanga ilishinda goli 1-0 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Timu zinaingia uwanjani.