×

Boeing Dreamliner Ndege ya Tanzania Itakayotua Nchini Julai

SERIKALI kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, imesema kuwa ndege mpya za Tanzania zitawasili nchini mwezi Julai mwaka huu ikiwemo Boeing Dreamliner

.

 

Dkt. Abbas amesema hayo leo Machi 5, 2018 akizungumza na wanahabari na kusema kuwa kwa sasa nguvu kubwa inafanywa kuendelea kupanua viwanja vya ndege nchini ili kuruhusu ndege hizo kuweza kutua katika viwanja mbalimbali.

 

“Julai mwaka huu nchi yetu itapokea ndege kadhaa mpya ikiwemo ‘Boeing Dreamliner’ hivyo ukarabati wa viwanja vya ndege vya Kitaifa/Kimataifa na Kimkoa unaendelea kwa kasi nchini. Meli mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria  1200 na mizigo tani 400 Ziwa Victoria, mkandarasi amepatikana na majadiliano ya mwisho na kusaini mkataba na kampuni ya STX ya Jamhuri ya Korea vitafanyika mwaka huu,” alisema Dkt. Hassan Abbas,