MBUNGE wa Nanyamba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdalah Chikota pamoja na waandishi wa habari watatu wa vyombo vya ITV, Clouds Media na Mwananchi, wamepata ajali katika eneo katikati ya vijiji vya Navikole na Chawi mkoani Mtwara.

Ajali hiyo imetokea baada ya gari lao kupinduka kama picha zainavyoonyesha ambapo hata hivyo hakuna majeruhi wala vifo.
Waandishi waliokuwemo ni pamoja na Juma Mohamed wa Clouds Tv, Merry Sanyiwa wa Mwananchi na Modestus Mwambe wa ITV.
Taarifa za awali zinaeleza watu wote waliohusika kwenye ajali hiyo wako salama wamepata gari lingine na sasa wanarejea Mtwara Mjini.