×

Nyota Shine wadata na studio za Global TV Online

Kundi la muziki linaloundwa na vijana watano machachari kutoka pande za Temeke jijini Dar, wamedatishwa ile mbaya na studio za Global TV Online zilizopo Sinza Mori baada ya kutinga kwa ajili ya kufanya mahojiano.

Akizungumza na mtandao huu, mmoja wa viongozi wa kundi hilo, Haime Bway alisema kuwa, mara kadhaa wamekuwa wakisikia tu sifa za studio hiyo lakini ilikuwa ngumu kuamini hadi pale walipofika na kujionea.

“Kusema ule ukweli hili ni bonge la studio, nasema hivyo kwa sababu nimejionea vifaa vya kisasa, mazingira ya kuvutia, yaani ukiingia unajiona kweli uko studio,” alisema Haime Bway.

Naye Dno Dyuzer kutoka studio za Ladha Records ambaye ni prodyuza wa wimbo mpya wa kundi hilo uitwao Cheza alisema: “Global TV nawapa big up sana, watangazaji wanafanya kazi nzuri ya kuwasaidia wanamuziki wa Bongo, Mungu awabariki sana. Lakini pia nawaomba Watanzania wawape sapoti vijana wangu. Nyota Shine limekuja kufunika, yaani vijana wamedhamiria kuliteka soko la muziki na kwa kusikiliza wimbo wa Cheza utaamini hiki ninachokuambia.”