
Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, kufuatia vifo vya watu 26 vilivyotokea Jumamosi saa tatu usiku baada ya basi dogo (Hiace) lililokuwa limebeba abiria kugongana na lori katika kijiji cha Mparange Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.
