×

Pluijm Atamba Kutwaa Kombe La FA

Kocha wa Singida United, Hans van Der Pluijm akiongea na wachezaji wake.

BAADA ya kuitoa Yanga katika nusu fainali ya Kombe la FA, Kocha wa Singida United, Hans van Der Pluijm ametamba kwa kusema atajipanga kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa michuano hiyo.

 

Singida iliitoa Yanga kwa penalti 4-2 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA uliochezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Pluijim ambaye ni raia wa Uholanzi, alisema lengo ni timu yake kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika mwakani kwa kukiandaa vizuri kikosi chake kuelekea nusu fainali.

 

“Lengo letu ni kupata nafasi ya kushiriki michuno ya kimataifa mwakani, nitakiandaa kikosi changu ili kifanye vizuri katika hatua ya nusu fainali. “Maandalizi yangu kwa sasa yanaangalia pande zote mbili yaani mechi za Ligi Kuu Bara na Kombe la FA, mechi zote hizo ni ngumu kutokana na ushindani uliokuwepo,” alisema Pluijm.

Singida United itacheza na JKT Tanzania katika nusu fainali ya Kombe la FA.

Stori: Khadija Mngwai