×

MAGUFULI AZINDUA KITUO CHA POLISI CHA KIDIPLOMASIA NA UTALII -VIDEO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Aprili 7, 2018 anazindua Kituo cha Polisi cha Kidiplomasia na Utalii jijini Arusha.

Kituo hiki kitakuwa na jukumu kubwa la kuwahudumia watalii, mabalozi na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu za serikali wa ndani na nje ya nchi hasa kuhusu masuala ya kidiplomasia.