×

Mahawe: Serikali Inapiga Kazi Bana, Juhudi Hizi si za Kubezwa – Video

MBUNGE wa Mkoa wa Manyara (CCM), Ester Alexeander Mahawe, ameipongeza wizara ya Tamisemi iliyopo chini ya Waziri Jaffo kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuboresha miundombinu hususani katika jimbo lake la Manyara.

 

Mahewa ameyasema hayo leo bungeni Mjini Dodoma na kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwapelekea Ambulance wananchi wake huku akipongeza pia jitihada za serikali kujenga ukuta katika migodi ya Mirerani ambayo itakuwa mwarobaini kwa wizi na utoroshwaji wa madini ya Tanzanite kutoka migodi hiyo. 

 

Aidha, Mahewa amesema serikali inafanya kazi nzuri na juhudi hizo si za kubezwa bali kuungwa mkono, pia amemuomba Waziri Jaffo kuweka mikakati ya haraka ya kumaliza tatizo la upungufu wa vyoo mashuleni.

Mahawe: Serikali Inapiga Kazi Bana, Juhudi Hizi si za Kubezwa