
KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude amesema mechi yao na Yanga itakuwa ngumu lakini kwao muhimu ni pointi tatu ili wajiweke katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Simba na Yanga zinakutana Jumapili wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo ambapo unatavuta hisia za watu wengi kufuatia kila upande kuhitaji ushindi.
Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 59 ikiwa imecheza mechi 25 huku Yanga ikiwa nafasi ya pili na pointi 49 ikicheza mechi 23. Zote zipo katika mbio za kuwania ubingwa.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mkude alisema wanahitaji kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo huo ili waibuke na pointi tatu.
“Mechi yetu na Yanga ni ngumu kwa sababu kila mmoja anajua ukubwa wa mchezo wenyewe ambao mara nyingi huwa na ushindani.
“Kikubwa tunachotakiwa kukifanya ni kupata sapoti na ushirikiano baina ya wachezaji katika mchezo huu ambapo uwezo wa timu kwa jumla ndiyo utakaoamua ushindi,” alisema Mkude.