Mbunge wa Mikumi kupitia Chadema, Joseph Haule, akichangia Mjadala wa ujenzi wa barabara uliopo katika bajeti ya wizara ya ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka 2018/19, iliyosomwa juzi na Waziri wake, Profesa Makame Mbarawa ameitaka serikali kufanya juhudi za ujenzi Barabara jimboni kwake ili kurahisisha shughuli za ufarisihsaji na kuinua uchumi wa eneo hilo.
Mbunge Joseph Haule ambaye ni msanii wa Hip Hop nchini, amemuomba Mwenyekiti wa Bunge hilo atumie staili ya kurap katika kuchangia hoja yake ili aweze kutumia Dakika tano ipasavyo.