×

MAMA KIKWETE: KIBA NA MKEO MSIPEKULIANE SIMU, MTAACHANA- VIDEO

MKE wa Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete alipata fursa ya kuhudhuria katika harusi ya staa wa Bongo Fleva, Alikiba na mkewe, Amina katika ukumbi wa Serena Hotel uliyopo Posta jijini Dar es Salaam jana usiku Aprili 29, 2018 na kutoa nasaha zake kwa maharusi hao.

“Ninawaombea maisha yenye amani na afya, lakini niwaombe waishi katika maisha ya kumcha Mungu. Leo ni siku ya raha kwenu, maisha haya ambayo mumeyaanza mkayaishi kwa raha.

“Simu ni mtihani na simu ni hatari, ukichukua simu ya mwenzako ukaanza kuikagua, mtaachana mapema kabla ya siku, nawaomba aminianeni, maisha yatakuwa mazuri,” alisema Mama Salma.

Mama Salma ambaye pia ni mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliambatana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Ummy Mwalimu katika seherehe hiyo.

Katika sherehe hiyo pia inahusisha harusi ya mdogo wa Alikiba, Abdu Kiba na mkewe, Ruwayda ambao walifunga ndoa Jumapili iliyopita.

TAZAMA VIDEO AKIFUNGUKA