×

ANTY  EZEKIEL KUZINDUA FILAMU YA ‘MAMA’ MEI 13

Anty Ezekiel akizungumza na waandishi wa habari leo Mei Mosi kuhusu uzinduzi wa filamu yake iitwayo ‘Mama’.
…Akitoa maelezo zaidi kuhusu filamu hiyo.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.

 

Msanii maarufu wa filamu nchini, Anty Ezekiel, anatarajia kuzindua filamu yake mpya aliyoipa jina la ‘Mama’, siku ya Jumapili Mei 13 mwaka huu yenye maudhui ya kuenzi na kutambua mchango wa mwanamke kama mama kwenye jamii,

 

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Anty  amesema kuwa ameamua kuonyesha umuhimu na thamani ya mwanamke katika jamii kutokana na nafasi ya mama.

 

Uzinduzi huo wa filamu hiyo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Mei 13 mwaka huu.

 

 

Na Denis Mtima/Gpl.