×

Kanyasu: Waziri Taja Wabunge Waliokamatwa Wakivua Samaki – Video

Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constatine Kanyasu amemtaka Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina kutaja majina ya wabunge wambao wameshakamatwa wakifanya uvuvi haramu ama dhana zao haramu za uvuvi kinyume na sheria.

 

Kanyasu ameyasema hayo bungeni wakati akichangia bajeti ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi na kusema Wizara hiyo amekuwa akisema kuna wabunge ambao wamekamatwa wakivua samaki au nyavu zao kukamatwa, hivyo Serikali haitaangalia cheo cha mtu au umaarufu wake, bali itamshughulikia kwa mujibu wa sheria za nchi.

 

“Kilio kikubwa cha wananchi ni unyang’anyi wa nyavu unaofanywa na wizara hii, tumekuwa tukihoji maswali hapa bungeni yanakuja majibu mepesi kwamba ‘tumekemata wabunge’ ndiyo maana wanalalamika. Sidhani na sina kumbukumbu  kama kuna mbunge alikamatwa akivua samaki au na dhana haramu za kuvulia, hili linatia uoga kwa wabunge kuchangia wakiogopa kutuhumiwa au kuambiwa wana maslahi binafsi.

 

“Ninaunga mkono oparesheni ya uvuvi haramu, lakini lazima kuwepo na mipaka, wanawenda kwenye mwalo, wanaangalia mtu mwenye mitumbwi mingi kama 30 hivi, wanamkamata, wanakamata nyavu zake na kumshikilia kwa siku nzima, wanamwambia alipe faini Tsh. Milioni 20, akikosa pesa hiyo wanamfungulia mashtaka au wanamfirisi.

 

“Pamoja na kutafuta pesa kwenye samaki, lakini samaki ni chakula, wafikirieni kwanza watu ambao wanategemea samaki kama chakula, huu ni uonevu. Mfanyabiashara amelipia nyavu, amelipia ushuru lakini anazuiliwa nyavu zake zisiingie, waziri amenyamza hasemi kitu, hivi mnataka watu wavue kwa kutumia nini? Nyavu imepanda kutoka Tsh. 16,000 hadi Tsh. 40,000,” alisema Kanyasu.

 

VIDEO: MSIKIE KANYASU AKIZUNGUMZA