×

NASHA: Serikali Haitahusika Kupanga Ada kwa Shule Binafsi – Video

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema haitajihusisha na upangaji wa ada kwa shule binafsi hapa nchini badala yake itasimamia elimu ili kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora kwa manufaa yake na taifa kwa ujumla.

 

Hayo yamesemwa leo Jumatatu, Mei 21, 2018 Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha wakati akijibu swali la msingi la Mbunge Viti Maalum, Mariam Kisangi​.

 

Aidha, Ole Nasha ameawataka wazazi kuwapeleka watoto wao katika shule hizo wakizingatia uwezo wa kipato chao ambacho kinawawezesha kumudu ada na gharama za shule hizoi ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza kwa wazazi hao ama kwa wamiliki wa shule.

MSIKIE OLE NASHA AKIFUNGUKA