
KIJANA Michael Rotondo (30), ameamriwa na Mahakama ya Onondaga, Syracue jijini News York Marekani kuhama nyumbani kwao baada ya wazazi wake kumfungulia mashtaka wakimtaka aondoke nyumbani hapo kwani amekuwa hachangii kodi ya nyumba wala gharama zozote nyumbani, na kwamba alikula pesa aliyopewa ili ahame.
Bi. Christina na Mark Rotondo walifungua shauri hilowiki iliyopita baada ya juhudi zao za kumuondoa kijana wao nyumbani ikiwemo kumpa dola za Marekani 1,100 na kumtaka auze baadhi ya vitu vyake ikiwemo gari yake mbovu aina ya Volkswagen Passat kugonga mwamba.
Licha ya kumuandikia barua mara tano kumtaka ahame nyumba yao Christina na Mark Rotondo wanasema mtoto wao huyo amekataa kuhama ambapo amedai kisheria hakupewa muda wa kutosha kumwezesha kuondoka.

“Tumeamua kuwa ni lazima uondoke nyumba hii mara moja,” barua moja iliyokuwa imeandikwa Februari 2, mwaka huu. Wakati Michael alipuuza barua hiyo, wazazi wake kupitia wakili wao, waliandika tena barua ya kumuagiza ahame kisha wakampa dola 1,100 kuondoka nyumbani pamoja na barua iliyokuwa na maneno makali kuhusu tabia yake wakimtaka kuuza baadhi ya vitu vyake ikiwa ni pamoja na gari aina ya Volkswagen Passat ambayo ilikuwa mbovu.
“Kuna ajira nyingi hata kwa wale walio na historia mbaya ya kazi kama wewe,” Tafuta moja – ni lazima ufanye kazi!” walisema.
Mpaka Machi 30, ilionekana wazi kuwa mtoto huyo hana mpango wowote wa kuondoka ndipo wakaamua kwenda mahakamani kuomba msaada wa nguvu ya sheria kumuondoa lakini mahakama hiyo iliwaeleza kwa sababu Michael ni mmoja wa watu wa familia watahitaji uamuzi wa mahakama ya juu zaidi kuweza kumhamisha.
Hata hivyo hakimu alimsifu Michael kwa utafiti bora wa kisheria lakini aliamuru kuondoka nyumbani huku Jaji Donald Greenwood akimwambia mahakama haiwezi kumruhusu kuendelea kubaki nyumbani kwa wazazi wake miezi sita miezi zaidi.

Rotondo, ambaye ambaye amekuwa akitegemea watu kwa msaada na alikuwa akijitetea mwenyewe mahakamani bila wakili, alisema ilikuwa ni notisi ya kufukuzwa ambayo ilikuwa mbaya. “Sioni kwa nini hawawezi tu kunivumilia kidogo nikaondoka nyumbani.
Rotondo alisema uhusiano na wazazi wake haujawa mzuri, kiasi cha kutozungumza kabisa ndani ya nyumba na kwamba wazazi wake walimwambia kuwa anaweza kuishi nao miaka minane iliyopita alipopoteza kazi lakini kwa sasa ana kazi, alipoulizwa kuhusu kazi anayofanya alikataa kutoa maelezo zaidi.
Aidha, Jaji alimsihi kuzungumza na wazazi wake na kwa hiari kuondoka nyumbani hapo, lakini Mr Rotondo alikataa. “Ninataka uondoke yumbani kwenu.”
Kijana huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa atakata rufaa, na amepanga kuondoka nyunbani miezi mitatu ijayo.