×

EXCLUSIVE: Akilimali Afunguka Atakavyotoa Mishahara kwa Wachezaji – Video

HAKUNA Asiyemfahamu Mzee Akilimali kutokana na umaarufu wake ndani ya Klabu ya Yanga ambako amekuwa akivutana na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo huku wakidai kuwa ndiyo anakwambia maendeleo ya klabu.

 

Jina lake halisi ni Ibrahim Akilimali, huyu ni Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga ambaye amekuwa akitoa maneno ya shombo kwa wachezaji au hata viongozi wa timu hiyo anapoona hawafanyi vizuri.

 

Siyo kwamba haipendi Yanga bali huyu ni Yanga lialia Lakini wapenzi wa soka nchini wamekuwa wakijiuliza mambo kadhaa kuhusiana na mzee huyo ambaye haishiwi vituko kila kukicha.

 

Global TV Online imefanya mahojiano maalum kujua mambo kadhaa muhimu kuhusiana na Klabu ya Yanga .