




BENKI ya NIC imewafuturisha baadhi ya wateja wake wa jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuboresha uhusiano na wateja.
Meneja wa idara ya wateja wadogo na taasisi wa benki hiyo, Natasha Cathles, akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika hoteli ya Hyatt Regency alisema anawashukuru wateja wa benki hiyo kote nchini kwa kuendelea kuiamini benki yao katika kupata bidhaa na huduma za kibenki zilizo bora.
Lengo la futari hiyo ni kukutana na wateja na kujadiliana jinsi ya kuboresha huduma zao.
“Siku ya leo ni muhimu kwetu hapa Dar es Salaam kwa kuwa tunafuturu pamoja na kutakiana mfungo mwema wa mwezi wa Ramadhani ambao unaendelea.
“Sisi kama Benki ya NIC, tunawatakia mfungo mwema wa Ramadhani lakini pia maandalizi mema ya sikukuu! Endeleeeni kufurahia huduma zetu mbalimbali na msiache kutembelea matawi yetu yaliyopo nchini,” alisema Cathles.