×

Aliyempa Wolper Jeuri ya Pesa na Gari la Mil. 170 Anaswa Live

UNAMKUMBUKA yule kigogo aliyewahi kumpa jeuri ya pesa mjini na kutanulia ule mkoko wa gharama aina ya BMW X6 mrembo wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper? Usipate tabu, anaitwa Abdallah Mtoro ‘Dallas’ na wikiendi iliyopita alinaswa kwenye mnuso wa futari na kuibua mshangao kwa watu.

Dallas alionekana kwenye viunga vya Mlimani City Ijumaa iliyopita kulipokuwa na futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

 

Akiwa kwenye viunga hivyo, Dallas aliwashangaza watu kutokana na muonekano wake na mambo ambayo alikuwa akiyafanya.

“Mh! Huyu Dallas jamani mbona kanenepa hivi? Halafu mbona anajiweka karibu sana na Makonda? Ona sasa pale anamfuata (Makonda) akiwa na watu kama anayesema achana nao hao njoo unisikikilize mimi,” mmoja wa wahudhuriaji wa hafla hiyo alisikika.

Paparazi wetu aliyekuwa akifuatilia matukio mbalimbali katika mnuso huo, alimfotoa picha kadhaa Dallas alipokuwa anamshika mkono Makonda na wakati alipokuwa anafuturu.

Kama hiyo haitoshi, paparazi wetu alimfotoa picha kadhaa akiwa ameshika ‘kasimu’ kadogo akiwa bize kuchatichati (haikufahamika anachati na nani).

“Huyu Dallas si wa kuchezea kasimu kadogo kama kale huyu si ndio aliyempa jeuri Wolper miaka ile? Kweli atakuwa hana simu ya kupangusa? Haiwezekani,” alisikika mhudhuriaji mwingine.

 

Hata hivyo Ijumaa Wikienda lilibaini ile simu aliyokuwa ameishika Dallas ni miongoni tu mwa simu zake, alionekana kuwa na simu nyingine kubwa.

Kabla ya kumwagana mwaka 2013, Wolper aliwahi kuwa na uhusiano mzito na Dallas ambaye alifahamika kama mfanyabiashara mwenye mkwanja mrefu mjini kabla ya kudaiwa kushuka kimkwanja.

 

Stori: Richard Bukos, Dar