×

SABA MBARONI KWA KUKUTWA NA SILAHA BILA VIBALI – VIDEO

JESHI la Polisi  Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na  Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) wamewakamata  watu saba  katika hifadhi  ya Saadan ambao  wakiwa  wanamiliki  silaha ambazo walikuwa  wakizitumia  kufanyia uwindaji  haramu   katika hifadhi hiyo  bila ya kuwa na kibali  huku  wakituhumiwa kumuua myama mmoja adimu anayepatikana kwenye hifadhi hiyo ya Saadan pekee    aliyemtaja kwa jina  Pongwe
Akizungumza na waandishi wa habari  Kamanda wa  Polisi  Mkoa wa  Pwani Jonathan Shanna amewataja watuhumiwa waliokamatwa  kuwa ni Hadija  Rashid ( 32 )mkazi wa Mkange   amekamatwa na Magobore mawili, Amina Athumani (30) mkazi wa Gama  amekamatwa na  risasi tisa  za Short Gun , Mohamed Athuman  (65) mkazi wa Manda  ambaye amekamatwa  magobore mawili Yusuph Salum( 62) ,pamoja  na Salum  Ramadhan( 96)mkazi wa  Manda amekamatwa na magobore  mawili.
Kamanda Shanna amewataja watuhumiwa wengine kuwa ni  Athumani Abdully (26), Siwatu Bakari(40) na Mussa  Abdully wote wakazi wa Manda  na walipokamatwa kila mmoja alikiwa na gobore moja.
Kufuatia tukio hilo Kamanda Shanna ametoa siku moja kwa raia wanaomiliki silaha isivyo halali kuzisalimisha mara moja.
Katika tukio la pili Jeshi  la Polisi  Mkoani hapa  wamekamata  gari lilikokuwa  limeibiwa  katika eneo la vigwaza  mapema mwaka huu lenye namba za usajili T.265 BZCaina ya  Mitsubish Canter tukio hilo lilitokea  baada ya kundi la watu sita  huku mmoja wao akijifanya ni mwalimu wa shule  ya sekondari Vigwaza akiwa na wenzake walimfuata dereva  aitwaye Omari Nyange(39) na kumwambia kwamba wanataka kumkodi ili wakahamishe vyombo dereva huyo alikubaliana na watu hao  na walipoanza safari ya kwenda eneo la Madafu walimbadilikia na kumkaba  kisha  kumpora  gari  hilo na yeye kumtupa nje.
Baada ya taarifa hizo kufika katika Jeshi la Polisiwalianza upelelezi na Juni 6 mwaha huu wakalikamata  katika Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro baada ya mwizi mmoja kukamatwa aliyetajwa kwa jina la Kasimu Nasoro(40) ambaye amekiri kuhusika na tukio hilo na kusema kuwa baada ya kuiba gari hilo walilibadilisha namba  na kufunga namba za bandia  ambazo ni T.525ABM na kulisafitisha hadi Mangula  ambako walitengeneza kadi bandia  na kwenda kuliuza  kwa kiasi cha Sh. 8,000,000 kwa Florida  Stanslaus  mkazi wa Mang’ula  Morogoro.
Katika tukio la tatu Jeshi la Polisi  katika mzani wa Msata Wilaya ya Kipolisi Chalinze wamekamata  madumu matupu ambayo yanadaiwa kukamata gari aina ya fuso lililokuwa linaendeshwa na dereva likiwa limebeba vyuma chakavu ambavyo havikulipiwa ushuru wa serikali ambapo walitozwa faini kiasi cha Sh. Mil. 2,000,000 na Maofisa  wa kuhifadhi na kutunza mazingira kwa kosa la kukwepa ushuru.

​Imeandaliwa na Khadijja Kalili Pwani.