Chama cha Wananchi CUF kimeendelea kuwa katika hali ya mvutano mkubwa wa uongozi wa chama hicho ambao umegawanyika katika makundi mawili, upande wa Maalim Seif Sharrif Hamad ambao sasa wanajiita CUF Taasisi na upande wa Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba.
Wabunge wanaomuunga mkono Maalim Seif wamejitokeza leo kuzungumza na waandishi wa habari ambapo wamemtaka msajili wa vyama vya siasa, Jaji Mutungi kujizulu kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kupuuza amri ya mahakama.