×

DULLY SYKES AFUNGUKA SIRI NYUMA YA WIMBO WA ZOOM

Abdul Sykes ‘Dully Sykes’

MKONGWE wa Muziki wa Bongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’, amefunguka kwamba miongoni mwa vitu watu wasivyofahamu nyuma ya ujio wake mpya wa Wimbo wa Zoom ni kwamba wimbo huo umemsumbua sana kwenye kurekodi.

Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Dully alisema wimbo wa Zoom, umemchukua takriban mwezi mmoja kuwa studio kwani alikuwa akirekodi na kuacha, kutokana na ziara zake za kimuziki.

“Nilikuwa nina ziara nyingi kiukweli za kimuziki, sasa wimbo wenyewe huu ulikuwa unahitaji utulivu wa hali ya juu. Kwa hiyo nilikuwa narekodi narudia tena, mpaka hivi umekamilika,” alisema Dully.

Hata hivyo, Mikito ilimuuliza pia Dully juu ya sababu za kufanya kazi na Prodyuza Mr. T-Touch na siyo studio yake ya 4. 12, alisema;

“Ukiwa mpishi unatakiwa kuonja pia mapishi ya watu wengine. Ni kweli nina studio lakini T-Touch, ni prodyuza mzuri pia. Sisemi kwamba, studio yangu hakuna prodyuza wazuri, lakini ni vile tu ninapenda kufanya kazi na T. “Lakini pia si kwamba kazi zote nitafanya naye, zipo nyingine nitafanyia kwenye studio yangu na nyingi nimefanyia kwangu pia.”

 

Stori: Boniphace Ngumije