The House of Favourite Newspapers

Gor Mahia Waleta Kikosi cha Pili Kagame Cup

MABINGWA mara mbili mfululizo wa SportPesa Super Cup, Gor Mahia FC ya Kenya, wamepanga kukitumia kikosi chao cha pili katika michuano ya Kombe la Kagame iliyopangwa kufanyika Juni 29, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, timu hiyo imepanga kuvigawa vikosi viwili kimoja kikiwepo Nairobi, Kenya kikijiandaa na mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Yanga.

 

“Gor Mahia italeta kikosi cha pili badala ya cha kwanza kwa lengo la kujiandaa na mechi ya Yanga itakayochezwa Julai 17, hivyo kikosi cha kwanza kitabaki na maandalizi Kenya na kingine cha pili kitakuja kucheza Kombe la Kagame,” alisema mtoa taarifa huyo.

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Comments are closed.