×

Maywether Anunua Saa, Bei Yake Mshahara wa Pogba Kwa Mwaka – Video

 

MFALME wa ngumi za kulipwa duniani kwa sasa, Floyd Weather,  ameendeleza kufuru yake ya pesa na kujiwekea rekodi zake za kununua bidhaa zenye gharama kubwa zaidi duniani. Ukiweka kando magari yake ya kifahari anayomiliki, nyumba na mali nyingi za mabilioni ya fedha, Mayweather amenunua saa mpya yenye gharama kubwa zaidi duniani.

Mayweather ambaye ndiye mwanamichezo anayeshikilia rekodi ya kulipwa mkwanja mrefu zaidi duniani kwa sasa akijikusanyia dola milioni 285 kwa mwaka (kwa mujibu wa Forbes), kupitia ukurasa wake wa Instagram,  ameanika saa hiyo iitwayo “The Billionaire Watch” huku akitaja gharama yake kuwa ni Dola za Marekani milioni $18 sawa na Euro milioni 15.58 (ambazo ni Tsh bilioni 40.2).

 

Saa hiyo imetengenezwa mwaka 2015 na kampuni ya Jacob & Co kwa madini ya almasi na kutajwa kuwa ndiyo saa yenye gharama zaidi duniani kwa sasa. Mayweather ameanika pia kwamba amenunua saa hiyo kwa sonara maarufu zaidi duniani, Mjapani, Tadashi Fukushima.

Lakini si hivyo tu, gharama ya saa hiyo ni sawa na mkwanja  anaolipwa Paul Pogba na Manchester United, kwa mwaka mzima. Pogba analipwa Euro milioni 15.08 kwa mwaka, lakini saa ya Maywether ni Euro milioni 15.58

 

Hata hivyo, rapa 50 Cent wa Marekani amemtukana Mayweather kwa kununua saa hiyo yenye gharama kama hiyo.

“Man they done found the 1 fool in the 🌎 world, dumb enough to buy that watch. LOL🤨get the strap,”ameandika 50 Cent kupitia Instagram.

#mood video credit: @moneyyaya Music by: @otgenasis

A post shared by Floyd Mayweather (@floydmayweather) on

@melissiarene

A post shared by Floyd Mayweather (@floydmayweather) on