
Beyonce (katikati) na mumewe Jay-Z wakiwa katika ziara yao Ulaya.
NYOTA wa muziki Beyonce juzi alishindwa kuteremka kwenye jukwaa maalum linaloinuka na kuteremka wakati anafanya shoo, yeye na mumewe, Jay-Z, jijini Warsaw, Poland, ambapo mafundi walimsaidia kumteremsha kutokana na mashine za jukwaa hilo kushindwa kufanya kazi.
Wanamuziki hao ambao wanafuatana na watoto wao watatu — Blue Ivy (6) na mapacha Rumi na Sir wenye umri wa mwaka mmoja, baada ya kumaliza ziara yao Ulaya magharibi, ya On the Run II, hivi sasa wako Ulaya Mashariki.