×

Taarifa Kuhusu Ratiba ya Kuaga Mwili wa Prof. Maji Marefu

MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Steven Ngonyani maarufu kama Profesa Maji Marefu, unatarajiwa kuagwa keso Jumatano kuanzia saa tatu jijini la Dar es Salaam na baadaye kusafirishwa kuelekea jimboni kwake Korogwe kwa ajili ya mazishi.

 

Mtoto wa Marehemu Thomas Steven Ngonyani amesema kuwa familia inasubiri taarifa rasmi kutoka serikalini kuhusu eneo ambalo ataagwa kwa Dar es Salaam.

 

“Kwa Dar es Salaam ataagwa kesho saa tatu na kuhusu ataagiwa wapi tunasubiri taarifa kutoka serikalini,” amesema Thomas.

Prof. Maji Marefu alifariki dunia jana, Juni 2, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alipokuwa akipatiwa matibabu na atazikwa keshokutwa Alhamisi Korogwe, Tanga.