×

ANACHOKIFANYA SANCHI NA MBWA

Jane Rimoy ‘Sanchi’

MWANAMITINDO maarufu ndani na nje ya nchi, Jane Rimoy ‘Sanchi’ amefunguka kuwa siku za hivi karibuni amekuwa akitumia muda wake mwingi sana kucheza na mbwa wake kwani anampa faraja anapokuwa nyumbani.

 

Akizungumza na Amani, Sanchi alisema mara nyingi mbwa wake huyo amemfundisha vitu vingi sana hivyo anaelewa chochote anachomwambia na anamfanya kuwa ‘bize’ kuhakikisha yuko msafi na anakula chakula kizuri.

 

“Napenda sana kucheza na mbwa wangu, nikiwa nimetulia tu nyumbani kama sina sehemu yoyote ya kwenda kazi yangu ni kukimbizana na mbwa wangu au kumpikia chakula chake na kujua usafi wa mwili wake ndicho kitu nachopenda sasa na ananipa faraja sana,” alisema Sanchi

Stori: Imelda Mtema, Amani