
WAZIRI Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa leo amewaongoza viongozi mbalimbali wa serikali, wabunge na waombolezaji wengine kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Hilary Ngonyani (Khalid) maarufu Maji Marefu katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Maji Marefu alifariki usiku wa kuamkia jana (Jumanne) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar alipokuwa akisumbuliwa na maradhi ya numonia.




PICHA: RICHARD BUKOS | GPL