WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya nchi, Kangi Lugola, amemfukuza kikaoni Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa kwa kuchelewa kufika kwenye kikao leo Julai 6, saa tano asubuhi ikiwa ni dakika chache baada ya kikao hicho kuanza.
Kabla ya kikao hico, Lugola litoa agizo kwamba ikifika saa 5:00 mlango wa ukumbi waliokuwa wakifanyia mikutano ufungwe, muda ulipowadia mlango huo ulifungwa kama alivyoagiza, lakini dakika moja baadaye (saa 5:01) mlango ulifunguliwa ili Dkt. Malewa aingie, mara baada ya kuingia, Lugola akahoji kwa nini amefunguliwa mlango? Licha ya Dk Malewa kuomba msamaha, Lugola aligoma na kumfukuza kwenye kikao hicho.

Aidha, katika kikao hicho, cha kimkakati cha viongozi wa vyombo na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo, Lugola ameagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, kumshusha cheo hadi kubaki na nyota tatu, Mkuu wa Usalama barabarani, Mbeya, Leopold Fungu huku akiagiza Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto mkoa wa Kagera, George Mrutu ashushwe cheo.